Diplomatic Briefing

Your exclusive news aggregator handpicked daily!

Archive for SWAHILI

Commentary: MABADILIKO YA TABIA NCHI: “Ni Waathirika Wakuu wa Kile Kitakachotokea”

Kikundi cha wazawa kimesafiri hadi hapa kwenye mazungumzo ya kihistoria kuhusu mabadiliko ya tabia nchi mjini Copenhagen kuonyesha wanaoendesha mazungumzo video za maisha halisi ambazo wametengeneza kuhusu madhara ya haraka ya mabadiliko ya tabia nchi katika nchi zao na katika maisha. “Tunataka kuonyesha watunga sera ukame wa miaka mitatu nchini mwangu unachokifanya kwa jumuiya zetu,” alisema Stanley Selian Konini, Mmasai kutoka Oltepesi katika wilaya ya Kajiado, Kenya.

http://www.ipsinternational.org/africa/sw/nota.asp?idnews=3168

Commentary: “Mataifa ya Kiafrika Yanahitaji Bodi ya Ushauri Nje ya Mazungumzo ya WTO”

Tangu kabla ya kuundwa kwa Shirika la Biashara Duniani (WTO) mwaka 1995, makundi mawili ya watu yamekuwa yakitofautina: wanaounga mkono biashara huria, ambao wanaona suala la kusaka maendeleo ni la msingi zaidi, na wapinzani wa biashara huria, ambao wanaona biashara isiyokuwa na vikwazo kama sababu ya matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi. Lakini tangu kuanza kwa mgogoro wa kiuchumi mwaka jana, kundi jipya linaanza kuibuka: wale wanaoamini mfumo wa zamani umekufa na wale wenye imani kuwa WTO inaweza kuchangia katika kupunguza umaskini na kuhifadhi mazingira, kama itafanyiwa mabadiliko. Au, ingerejea katika mamlaka yake ya awali.

http://www.ipsinternational.org/africa/sw/nota.asp?idnews=3156